Tanzia: Pigo Tena Bongo Movie, Muigizaji Haji Jumbe Afariki Dunia
Muigizaji wa tamsthilia hapa Bongo, Haji Jumbe, ambaye amekuwa akiigiza kama Mr. Benson katika tamthilia ya Siri za Familia inayorushwa na EATV amefariki dunia jana Jumatatu jioni, Oktoba 24, katika Hospitali ya Kinondoni kwa Dr. Mvungi.
Imearifiwa kuwa, siku chache kabla ya kifo chache, zilizopita alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo.
Mazishi yanatarajia kufanyika leo Jumanne majira ya saa 9:00 Alasiri, huko Bagamoyo, Pwani.