Bond: Watoto Wa Wastara Hawakupenda Aolewe
SIKU chache baada ya kuripotiwa kupika na kupakua na staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, Bond Suleiman ameibuka na kusema watoto wa mke huyo wa zamani wa Mbunge wa Donge, Sadifa Juma, hawakupenda mama yao aolewe na mtu mwingine zaidi yake.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Bond alisema alipokuwa kwenye ndoa, watoto hao walimfuata na kumwambia kuwa hawakufurahishwa mama yao kuolewa na mtu mwingine kwa sababu ya mapenzi ya dhati aliyokuwa akimuonesha mama yao enzi za uhusiano wao.
“Upendo wangu ndiyo uliomrudisha Wastara maana niliamua kubadilika na kuachana na pombe kwa ajili yake, nawaomba wanawake wanaonisumbua kunitaka kimapenzi waache kwani ninaye Wastara, mwanamke wa maisha yangu, siwezi kumsaliti tena, ndani ya mwaka huu tutafunga ndoa,” alisema Bond ambaye pia ni muigizaji.
Chanzo:GPL