-->

Barafu Aiponda Biashara ya Bongo Movie

Msanii wa Bongo Movie Barafu amesema biashara ya movie ni kama biashara kichaa kwa kuwa inamlazimu msanii kufanya kazi na kuipeleka kwa “Mhindi” ambaye hadi auze kwanza arudishe pesa ndipo amlipe msanii.

barafu

Barafu, Msanii wa Bongo Movie

Akiongea na eNewz Barafu amesema “biashara ya move ni tofauti na mtu anayeuza pipi au duka kwa kuwa unatengeneza movie kwa mamilioni lakini ukimaliza unaenda kukopesha msambazaji mpaka auze yeye ndo atulipe sisi kwa sasa ni mtu mmoja tu anaamuua kuwakoroga wasanii akisema movie haziuzi basi”.

Akiendelea kuongelea utaratibu wa uuzaji wa movie Barafu amesema kwa sasa yeye hafanyi tena kazi za movie za kukopesha, anataka afanye kazi halafu auze kwa msambazaji akasambaze na hakimiliki ibaki kwake tofauti na sasa ambapo amesema wasambazaji wanataka msanii awapatie hakimiliki pamoja na movie.

eatv.tv

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364