Baraka Afunguka Kuhusu Ndoa ya Mr. Blue
Msanii Baraka The Prince amezungumzia sakata la mpenzi wake Najma na Mr. Blue ambaye alikuwa mpenzi wake, na kusema tukio hilo halikuwa na ukweli wowote na hata kama lingekuwepo, hawezi kuzuia wawili hao kuwasiliana.
Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Fleva Top 20 cha East Africa Radio, Baraka amesema yeye hawezi kuzuia wawili hao kuwasiliana kwani wote ni wasanii, na pia hana kawaida ya kushika simu ya mpenzi wake na kujua amewasiliana na nani.
“Hamna zile stori sio za kweli, hata mimi Blue alivyoniface nilimwambia sijui hizo habari na sijawahi kuona ukimpigia, hata ukimpigia we ni mwanamuziki mwenzake, mi siwezi nikamuwekea mipaka Najma, au eti siwezi kuwekea mipaka hey Bro usimpigie Najma, kwanza mi hata kugusa tu simu ya Najma sijawahi na hata Najma kugusa simu yangu hagusi yangu, haijawahi kutokea tu kitu kama hicho sasa sijui kilitokea wapi”, alisema Baraka the Prince.
Baraka aliendelea kusema ingawa tukio hilo liliathiri kwa upande mwengine, lakini alijaribu kukaa na Mr. Blue kumshauri kuyapuuzia masuala hayo, na amtulize mkewe asisikilize ya watu.
“Mi nilimuelewa Blue kwa sababu Blue alikuwa analalamika kweli kwamba mwanamke wake anammind, kwenye familia yake hamna amani, mi niliheshimu kwa sababu najua haya mambo yalivyo, lakini mi nilijaribu kuongea naye nikamwambia amwambie shemeji atulie sio kweli bwana”, alisema Baraka the Prince.
eatv.tv