Baraka Akiri Naj Kumpoteza Kwenye Media
MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Baraka The Prince’ hivi karibuni amekiri kuwa, mpenzi wake wa sasa Najma Dattan ‘Naj’ ndiye amesababisha akauke kwenye vyombo vya habari ‘media’.
Akichonga na Mikito Nusunusu, Baraka alisema kuwa kipindi cha nyuma kabla hajawa kwenye uhusiano na Naj alikuwa hajatulia hivyo wasichana wengi walikuwa karibu yake na kujikuta mara kwa mara akiwa gumzo kwenye media lakini sasa hivi katulia na Naj, hana skendo za kuripotiwa hovyo tena.
“Unajua hakuna kitu kizuri kama kuwa na uhusiano uliokomaa, uhusiano wangu na Naj ni wa nguvu na nakiri kweli ameniweka mbali na media kwa skendo za ajabu, kwa sasa nawaza kazi na ninafurahia maisha haya,” alisema Baraka.
Chanzo:GPL