-->

Linah Sanga Afungukia Kuachia Tumbo Wazi

Linah Sanga ‘Ndege Mnana’ amefunguka na kuweka wazi kwamba haoni tatizo yeye kupiga picha za kuachia tumbo lake lenye ujauzito wazi kwani picha ni za kawaida sana wala hazina matatizo yoyote.

Linah Sanga ‘Ndege Mnana’

Linnah amefunguka hayo kwenye kamera za eNewz na kudai kwamba hawezi kumfurahisha kila mmoja ndio maana anafanya kile ambacho anahisi kipo sahihi kwa upande wake huku akidai wakosoaji wapo wengi.

“Zile picha mimi sioni tatizo lolote ingawa mimi siyo mtu wa kwanza kuziweka mtandaoni, Kwenye picha zile nimezaa vitenge na sehemu nyingine nimejisitiri kawaida kama ni kufuata maadili ya ki Afrika basi nivae majani kama jinsi zamani watu walivyokuwa wanavaa. Watu wanapenda sana kukosoa  nikivaa gauni wanasema navaa ki bibi, suruali nambana mtoto huwezi kuwazuia watu wasiongee kwa sababu kuna watu ambao watakuona upo wrong na wengine watakuona upo sahihi” alisema Linnah

Aidha Linnah ameongeza kwamba ‘comment za vichambo na matusi anazorushiwa na mashabiki hazimuumizi kwa kuwa yeye siyo mtu wa kwanza kuambiwa maneno makali bali wapo waatu wengi wanaopitia changamoto mbalimbali.

Linah Sanga ‘Ndege Mnana’

EATV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364