Barakah Da Prince Ajiweka kwa Naj
Msanii wa Bongo Fleva ‘Barakah da Prince’ akiwa na mpenzi wake Najma Dattan ‘Naj’.
HATIMAYE! Baada ya kufichaficha kila sehemu juu ya uhusiano wao, msanii wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ ameamua ‘kujilipua’ kwa mpenzi wake mpya, Najma Dattan ‘Naj’ na kwamba ndiyo kila kitu kwake.
Akiliachia domo liserereke, Barakah anayebamba na Ngoma ya Siwezi alisema kuwa japokuwa amekuwa akifuatwa na vyombo vingi vya habari kujua ukweli sasa imefika wakati wa kutoa tamko.
“Ujue siku zote nilikuwa sijapata mtu sahihi katika maisha yangu. Nimempata Naj na naamini kwa asilimia zote ana maono ya mbele tofauti na wote niliowahi kuwa nao, pili tunaendana kwa kila kitu na mwisho ni mshauri wangu hivyo sioni sababu ya kuficha,” alisema Barakah.
Chanzo: GPL