-->

RAY: Ningeteuliwa Waziri Ningeanza Kuwachuja Wasanii

MKONGWE wa filamu Nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’, amefunguka kuwa kama angeteuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, angeanzisha mpango maalumu wa kuwachuja wasanii.

Akiongea na +225 Kipindi cha XXL cha Clouds Fm amedai kuwa kila mtu anataka kuwa msanii, hakuna mgawanyiko wa kazi. Msanii akicheza filamu moja basi kesho ameshakuwa staa na anavaa kofia zote kama vile utayarishaji, uongozaji na uigizaji.

Ray amekerwa sana na jambo hilo pia amemshauri Dk. Harrison Mwakyembe kuwa aliangazie soko la filamu Bongo kwani sinema za kizungu zinauzwa shilingi 700 na filamu za hapa Bongo ni shilingi 2500.

Ray amedai kuwa filamu hizo zinauzwa gharama hiyo kwa kuwa zinauzwa bila ya kulipiwa kodi.

Salum Milongo/GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364