-->

Barnaba: Bado nampenda mke wangu

KUNA wasanii na wanamuziki. Wasanii ni wale ambao wanaweza kuifanya kazi yao kuwa sanaa na kuwapatia fedha. Kwenye kuimba wanaweza kuwa siyo wazuri sana.

Wanamuziki ni wale wanaojua kuimba. Wanafahamu ala za muziki, wanatengeneza mahadhi ya muziki wenyewe na kuimba kwa mvuto wa kipekee.

Kwa wale wa Bongo Fleva, kuna mtu anaitwa Barnaba. Huyu ni mwanamuziki. Anajua muziki kuliko kitu kingine chochote.

Amewahi kutamba na vibao kadhaa kama Wrongo Number, Magumegume, Lover Boy na nyinginezo. Kwa sasa ametoa kibao kingine kipya kinaitwa Mapenzi Jeneza.

Mwanaspoti limemnasa Barnaba katika maeneo fulani hivi na kumbananisha na kuzungumza naye machache. Mahojiano hayo yalikuwa kama hivi.

Mwanaspoti: Una watoto wangapi?

Barnaba: Nina watoto wawili, wa kwanza Steve na wa pili Maria, wengi najua hawafahamu hili.

Mwanaspoti: Ni kitu gani mashabiki zako hawakijui katika muziki wako?

Barnaba: Kitu ambacho hawakijui ni kuwa Barnaba hafanyi muziki kwa mashindano, hata siku moja.

Mwanaspoti: Mbali muziki unapenda kitu gani kingine?

Barnaba: Napenda kuangalia Movie (filamu), yaani ndani kwangu kuna filamu za Bongo, hasa za vichekesho, hadi mwanangu Steve nimempa jina hilo kutokana na kile alichokuwa akifanya marehemu Steven Kanumba.

Mwanaspoti: Kuna pengo lolote umelipata baada ya kuachana na mama steve?

Barnaba: Hakuna pengo la aina yeyote, ila upendo kwake umebaki pale pale japo tayari ana mwanamume mwingine.

Mwanaspoti: Ni kitu gani ambacho uliwahi kukifanya na hutaki kijirudie?

Barnaba: Kukaa na mwanamke kwa muda mrefu bila ya kumuoa, maana wanawake sio watu wa kushindana nao, muda wote wanabadirika.

Mwanaspoti: Malengo gani uliyapanga yakavurugika?

Barnaba: Kuwa na watoto mama tofauti tofauti.

Mwanaspoti: We mtoto wa ngapi kuzaliwa kwenu?

Barnaba: Mimi ni wa kwanza na tuko wa tatu kwetu.

Mwanaspoti: Kwa nini mara nyingi gitaa lako huliachi hata unapokuwa kwenye matembezi ya kawaida tu?

Barnaba: Gitaa limekuwa ni sehemu ya maisha yangu ya kila siku na mwanamuziki wa kweli kabisa lazima apende gitaa kwa sababu linakuwa na hisia za muziki wa ndani kabisa. Kwa kweli kwangu bila hilo naona sijafanya kitu.

Mwanaspoti: Ulitamani kufanya nini utakapokuwa na mafanikio?

Barnaba: Nilitamani mama yangu angekuwepo ili aone mafanikio yangu kwa sababu alinisaidia sana.

Mwanaspoti

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364