-->

Barnaba: Bora Tuibiwe na Diamond

Barnaba amedai kuwa ni bora fedha zao za muziki ziibiwe na Diamond kupitia tovuti yake ya kuuza muziki ya Wasafi.com kuliko watu wengine.

Muimbaji huyo ameiambia Dizzim Online, “Tumeibiwa sana wasanii, tumedhulumiwa sana. Mungu anisamehe kidogo, bora atuibie msanii mwenzetu, tunajua msanii mwenzetu anakula yupo kwenye soko letu kuliko atuibie mtu binafsi.”

“Na yeye akiwa kama CEO [Diamond] alichukua uamuzi wa busara kama heshima kutupigia simu wasanii wenzake mwenyewe kuliko kuwatuma menejimenti. Mimi naona jambo zuri la bahati alilolifanya na nilienda nikachukuwa contract yangu na kiukweli nimeusaini lakini bado kuurudisha,” ameongeza.

Katika hatua nyingine hitmaker huyo wa ‘Lover Boy’ amewataja wasanii ambao watasikika kwenye albamu yake mpya. Wasanii hao ni pamoja na Baraka The Prince, Linex, Dela, H_art The Band, Bahati wa Kenya, Vanessa Mdee kuna Jux, Maua Sama, G Nako na wengine.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364