-->

Bashe, Musukuma, Malima Mbaroni

Dodoma. Wabunge wawili na aliyekuwa naibu waziri wa fedha, Adam Malima wanahojiwa na polisi mjini hapa kwa kosa la kutaka kufanya vurugu na uchochezi katika vikao vya CCM.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibisha na kuwataja waliokamatwa kuwa ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Geita vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma na Malima.

“Hao ndio waliokamatwa na bado tunaendelea na mahojiano na wengine bado tunaendelea kuwatafuta,”amesema Mambosasa.

Amesema taarifa zaidi atazitoa baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika.

By Sharon Sauwa, Mwananchi ssauwa@mwananchi.co.tz

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364