Batuli: Sina Tatizo na Uwoya
Mwanamama wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ameweka wazi kuwa hana tatizo na mwigizaji mwenzake, Irene Uwoya labda aulizwe yeye (Uwoya) kwani anasikia tu watu wakisema kuwa ana bifu naye.
Batuli aliliambia Wikienda kuwa, anachojua yeye hana ugomvi na Uwoya na wala hana muda wa kusoma mitandaoni lakini angeomba aulizwe Uwoya.
“Sina muda wa kugombana na Uwoya, kama kuna tatizo aulizwe yeye siwezi kuusemea moyo wake,” alisema Batuli. Alipotafutwa Uwoya, kilongalonga chake kiliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa SMS hakujibu ingawa ujumbe ulionesha kuwa ameusoma.
Chanzo:GPL