Bi Mwenda Aukubali Uzee
DAR ES SALAAM: Mwigizaji mkongwe wa sinema za Kibongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ sasa ameukubali uzee baada ya kusumbuliwa na miguu ambayo imempunguzia kasi ya kufanya kazi zake za sanaa.
Akizungumza na Wikienda , Bi Mwenda alisema kuwa, sasa uzee ndiyo umekamilika kwani anasumbuliwa na miguu lakini anashukuru Mungu mambo yanakwenda vizuri.
“Nilipenda kutania uzee mwisho Chalinze lakini kiukweli sasa nimeukubali kwa sababu wala sina pa kukimbilia, miguu imeshanionesha kuwa nimezeeka,” alisema Bi Mwenda.
Chanzo:GPL