-->

Bond Afungukia Kukamatwa Kwake

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Bond Bin Suleiman, amefungukia kukamatwa kwake kwenye ishu ya ujambazi na kudai kuwa aliponzwa na rafi ki yake aliyekuwa hafahamu anajishughulisha na kazi gani.

Akizungumza na Wikienda, Bond alisema kuwa, yeye ni msanii na anakutana na watu wengi kama ilivyo kwa wasanii na kilichomkuta kinaweza kumkuta msanii yeyote kwani hukutana na watu wa aina zote hasa kwenye mambo ya starehe.

Bond Bin Suleiman

“Unajua mtu akikuita akakuambia twende tukanywe au njoo nikupe ofa si rahisi kuichunguza kazi yake na kama unavyojua watu hawa hufi cha sana mambo yao.

Huyo jamaa anayetajwa alikuwa ni mtu wa kuniita na kunipa kinywaji na si mara kwa mara lakini nashangaa watu wanavyoongea kuhusiana na jambo hilo zito ambalo likimkuta mtu yeyote si rahisi kulimaliza lakini nashukuru sina kesi ya kujibu na mambo yameisha, Watanzania wajue tu sijawahi kuwa mtu wa kazi hiyo ya ujambazi,” alisema Bond.

Bond alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kufanya kazi yao kikamilifu na kuamua kumuachia kwani haikuwa kesi rahisi na imeharibu sifa yake.

Kwa upande wa Wastara ambaye ni mpenzi wake alisema kuwa haogopi maneno ya watu kwani wanaongea sana lakini ukweli upo polisi na kama kungekuwa na kitu kama hicho, Bond asingeachiwa kirahisi.

Chanzo;GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364