-->

Bongo Muvi Hatujielewi-Lulu

Msanii wa maigizo aliyefanya vizuri na filamu ya ‘Mapenzi ya Mungu’, Elizabeth Michael ‘ Lulu’ amefunguka na kusema wasanii wa maigizo bongo wanafeli kutokana na kutojielewa ni kitu gani ambacho wanakitaka kwenye sanaa, badala yake wanafuata mikumbo.

Lulu amefunguka hayo hivi karibuni akizungumza na wanahabari na kusema kuwa wasanii wengi wa Tanzania hawapendi kujishughulisha kutafuta kitu kizuri kwa kuwa wengi wao walifuata mkumbo kwenye kuigiza  na wengine walichukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu ili maisha yaendelee au sehemu ya kupotezea muda.

“Ukweli upo kwenye uigizaji kuna watu tunachukulia hii ni kazi, wapo wanaofanya kama sehemu ya kipaji chake lakini pia wapo ambao wanachukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu au ku-refresh kwani wanakua na kazi zao zingine,  na hao ndio wanaosababisha tuonekane waigizaji wa muvi tumefeli”. 

Pamoja na hayo Lulu ameongeza, “Unajua pia kufuata mkumbo ni kitu kilichoturudisha nyuma. Watu wengi walikuwa wanaangalia mafanikio ya mtu mmoja na wote tukawa tunapita njia zilezile ili tufanikiwe badala ya kutafuta za kwetu ndiyo kama mnavyoona sasa hivi tunalalamika lakini mashabiki zetu wanatusapoti hivyo japo tunawakwaza”.

Akizungumzia kuhusu wasanii wa Nigeria walivyoweza kufanikiwa katika filamu zao, Lulu amesema ni pamoja na upendo na ushirikiano wanaoonyeshana katika kazi zao na kuongeza kwamba pamoja na kufanya kazi zenye ubora wa kimataifa watu hao hawajasahau utamaduni wao.

Kuhusu sababu za wasanii wa filamu kutokaa ‘Location’ kwa muda mfupi kutengeneza filamu zao kwa usahii muingizaji Lulu amefunguka na kusema changamoto kubwa huwa ni bajeti kwa wasanii hao.

“Bajeti zetu ni tatizo. Bado hatujawa na uwezo wa kuweka bajeti kubwa kwenye filamu ndiyo maana tunaomba tuwezeshwe ili tufanye kazi zenye ubora. Kuna vitu ambavyo sisi pia tunavifanya kwa mapungufu kwa sababu hatuna uwezo wa kumpatia pesa mtu sahihi wa kufanya kazi husika ndiyo maana unakuta tunafanya kazi kwa uwezo wetu tu. 

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364