-->

Chiki ‘Ampigia Magoti’ JB

Msanii wa bongo movie  Chiki Mchoma amesema JB hana sababu ya kustaafu kuigiza kwa kuwa ni mtu ambaye bado sanaa inamuhitaji na kuna wasanii wachanga na wakongwe wanamuhitaji kwa ushauri zaidi.

chiki

Chiki Mchoma

Akiongea kupitia eNewz Chiki amesema anamkumbusha JB kurudi bongo movie kwa kuwa sanaa haina kustaafu na kama kuna malengo ambayo aliyaweka yakawa hayajatimia asikate tamaa arudi kuendeleza chipukizi ambao wanakuwa lakini pia kama malengo yake yametimia basi awasaidie na waliopo chini yake.

Pia Chiki amesema hana mpango wa kustaafu kuigiza kwa kuwa anaamini kuwa kuna mashabiki zake ambao bado wanatamani kuona kazi zake na wanamkubali lakini pia anajipanga ili kuirudisha bongo movie kama zamani.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364