Wakati Zari Akitarajiwa Kujifungua Muda Wowote, Meseji ya Kumkaribisha ChibuJr Zatawala Mitandaoni
Wakati mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan akiwa ‘leba’ tayari kwa kujifungua mtoto wa pili wa kiume kwa nyota huyo, meseji mbalimbali zikiambatana na picha zimezidi kutrend kupitia mitandao ya kijamii hasa Instagram nyingi zikimtakia heri katika zoezi hilo.
Zari aliyepelekwa ‘leba’ jana katika Hospitali ya Netcare Pretoria iliyopo jijini Pretoria nchini Afrika Kusini anatarajia kujifungua wakati wowote.
Diamond, mama yake mzazi na ndugu zake wameendelea kumuombea Zari ajifungue salama mtoto huyo wa kiume.
Chanzo:GPL