-->

Christian Bella Afungukia Changamoto Aliyoipata Kwenye Kazi ya Fid Q

Msanii nguli wa kuimba mwenye asili ya Kongo na makazi yake hapa Bongo,Christian Bella , amesema amepata shida sana kwenye kurekodi wimbo wa msanii wa Hip Hop Fid Q, kutokana na ugumu wa mashairi yake.

bellaa32

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Christian Bella amesema ilimbidi aombe atafsiriwe maana ya maneno ya kwenye mashairi ya wimbo wa ‘roho’ wa Fid Q, ili aweze kuandika maneno ya kuimba kwenye chorus yake, hata hivyo aligonga mwamba.

“Nilipoambiwa niende nikapige chorus kwenye ngoma ya Fid Q ambayo alikuwa anarekodi pale kwa P Funk Majani, nikapiga mahesabu nikajua jamaa hip hop yake ngumu yani hata sijui itakuwaje, kwa sababu namuheshimu sana pia namkubali kwa hiyo itabidi niende tu, kwa hiyo nilipofika pale mistari yake nikisikiliza mi mwenyewe nashindwa hata kuelewa anaimba nini, kusema ukweli nilikuwa simuelewi jamaa, ana mashairi flan mpaka wakufafanulie vizuri ili nielewe, nikatengeneza melody lakini ilibidi nimuombe maneno akanisaidia”

Christian Bella aliendelea kusema kuwa msanii huyo tungo zake ni ngumu kuzielewa mara moja, na kwamba ndiyo kitu kilichompa ugumu kwenye kurekodi collabo yao, ambayo inafanya vizuri kwenye media za bongo sasa hivi.

“Anachana vitu ambavyo mi nilikuwa sielewi namuuliza hii ni nini unasemaje hapa!? Kwa hiyo nipe maneno basi tuendane ili nisiimbe maneno tofauti na mashairi yako”, alisema Christian Bella.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364