-->

Nuh Mziwanda Kuja na Khadja Kopa

Msani Nuh Mziwanda amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya mwakani 2017 na kusema kuwa tayari mpaka sasa amejipanga na ngoma kibao kali.

Nuh Mziwanda akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo alisema kuwa anatambua kuwa mashabiki zake wanasubiri ngoma mpya lakini kwa mwaka huu hataweza kuachia kazi mpka mwezi wa kwanza ambapo ataachia kazi yake mpya akiwa na Khadja Kopa.

“Kiukweli nina kazi nyingi ndani zote kali lakini mpaka sasa ushindani upo kwenye kazi mbili, kuna kazi moja nimefanya na Khadja Kopa inaitwa ‘Mtaa wa Kongo’ ndiyo nayo tegemea kuachia baada ya Jike Shupa, hiyo kazi nitaachia mwezi wa kwanza kwenye tarehe 20 hivi maana saizi ni kama nimechelewa. Najua kuna watu ambao wanasubiri niaachie ngoma nifeli lakini kiukweli mimi nawaamini sana mashabiki zangu ambao wanasimama na mimi siku zote”. Alisema Nuh Mziwanda.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364