-->

Chuchu Hans Adaiwa Kunasa Ujauzito

STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans anadaiwa kunasa ujauzito wa mchumba wake ambaye naye ni staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’.

RAY323

Chuchu na Ray

Kwa mujibu wa chanzo ambacho kipo karibu na wawili hao, Chuchu kwa sasa ni mtu wa kujifungia ndani na amekuwa hapatikani kwenye matukio mbalimbali yanayomhusu. “Ameshanasa, tena ujauzito huo ni wa Ray, unaambiwa sasa hivi kawa mtu wa kujifungia ndani tu na kitumbo kimeshamtoka,” kilisema chanzo.

Alipotafutwa Chuchu kujua ukweli alijibu; “Nashangaa, watu wengi wananifikiria hivyo lakini sitaki kuongea chochote. Labda watakuwa na husda tu ndiyo maana wananifikiria hivi,” alisema Chuchu. Ray alipotafutwa kwa njia ya simu ili kusikia kauli yake hakupokea

 

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364