Diamond Platnumz Atoa Msada wa Madawati 600
Msanii Diamond Platnumz akiwa na uongozi na wasanii wote wa WCB, leo wamemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda madawati 600 ya wanafunzi ambayo yatasaidia takribani ya wanafunzi 1800 katika jiji la Dar es Salaam ambao walikuwa wanakaa chini.
“Mapema leo na familia nzima ya WCB wasafi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda tulivyoenda kumkabidhi Madawati 600 kwajili ya Wanafunzi wa shule za Dar es Salaam. Madawati hayo ambayo yataweza kusaidia Wanafunzi elfu moja na mia nane kutoka kwenye kukaa chini na kuweza kukaa kwenye dawati na kupata elimu Vyema” Diamond aliandika kwenye ukurasa wake mtandaoni.