-->

Cloud afunga ndoa tena Ulaya kwa siri

NYOTA wa sinema za Bongo, Issa Mussa ‘Cloud’ amefunga ndoa  tena, lakini safari hii ni kwa siri huko nchini Sweden na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mina ambaye amekuwa akimposti kila kukicha mitandaoni kwa kumuita pacha.

CLOUD67

Chanzo kilicho karibu na staa huyo kililiambia gazeti hili kuwa, Cloud amemfanyia mbaya mkewe, Cynthia kwa kuamua kuoa kwa siri wakati imani yake inamruhusu kuwa muwazi.
Chanzo kilisema kuwa, awali Cloud alimwambia mkewe wa Bongo kuwa, amepata mfadhili hivyo anakwenda nchini Comoro kupata matibabu ya moyo ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

SIKIA HII MWENYEWE
“Hivi mnajua kuwa, msanii Cloud ana mke mwingine nchini Sweden, lakini mkewe Cynthia hapa Bongo hajui kwa sababu si mtu wa kujichanganya na watu na hata kwenye mitandao huwa haingii hovyo ka’ vile mumewe alimpiga stop.

“Fuatilieni kwenye akaunti yake ya Facebook. Huko ndiyo anatupia picha mbalimbali akiwa na huyo mwanamke ambaye anamuita pacha. Wameshafungua mgahawa na inavyosemekana Cloud ndiye anasimamia kwa sababu mkewe huyo anafanya kazi ya uuguzi.

“Lawama za sasa ni kwa nini Cloud hajisikii tabu kumuacha mkewe huku Bongo na hajawasiliana naye tangu aliposema anakwenda Comoro kumbe yupo Sweden. Kwa sasa mkewe ameamua kurudi nyumbani kwao baada ya kugundua kuwa, mwenzake ameoa tena huko,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya habari hizi kutua dawatini, Ijumaa lilimtafuta Cloud kupitia akaunti yake na kumuandikia madai hayo ambapo alikaa kimya bila kutoa majibu.

Ijumaa halikukata tamaa, lilikaa kwa muda wa mwezi mmoja likamtafuta tena kwa kumuandikia ujumbe kupitia akaunti yake hiyohiyo ambayo iko hai lakini pia hakujibu.

Juzi, Ijumaa lilimtafuta hewani mkewe Cynthia ambaye aliongea mambo mengi kuhusu madai hayo.
Ijumaa: “Cynthia za siku? Habari hizi ninazozisikia ni za kweli?”

Cynthia: “Habari gani ndugu yangu? Si unajua huwa sipendi sana mambo ya magazeti!”
Ijumaa: “Usinifiche kitu wakati mambo yako wazi. Ni kweli Cloud ameoa huko Sweden?”
Cynthia: “Nakuheshimu sana ndiyo maana naongea na wewe. Ni kweli ameoa ila mimi sikujua kwa sababu kama unavyomjua Cloud ni mtu ambaye ana mahaba sana. Aliniambia anakwenda kutibiwa Comoro nimuombee dua, tukaagana kwa uchungu huku tukilia na mabusu tele, kumbe anakwenda Sweden kuoa. Huwezi amini hata paspoti nilimtafutia mimi. Hivi ninavyozungumza na wewe sijaongea naye yapata mwaka mmoja sasa.”

cloud45

Ijumaa: “Wewe ulijuaje ameoa? Kwa sababu hakukwambia na inasemekana kwamba huwa haupo kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu alikukataza?”
Cynthia: “Ni kweli  alinikataza na nilikubaliana naye kwa sababu nilikuwa nikifuata amri ya mume na nilihisi ni wivu ndiyo ulimfanya anikataze kuingia kwenye mitandao kumbe alikuwa akificha mambo yake.

“Siku moja marafiki, jamaa na baadhi ya ndugu walinieleza kila kitu na kuniambia kwamba, walikuwa wakitamani kunivujishia siku nyingi lakini walikuwa wakinionea huruma kwa vile nilikuwa nawahimiza kumuombea mume wangu ili apone, arudi nyumbani tuendelee na kazi za filamu.”
Ijumaa: “Baada ya kujua ulimuuliza? Je, alikukubalia kuwa ameoa?”

Cynthia: “Nilikasirika kwa sababu wakati anaondoka alinidanganya na mimi nilikuwa nikiwahimiza watu tumuombee dua apone. Alikuja Tanzania kabla ya kuondoka kwa mara ya pili na kukiri kuwa alioa tukayaongea yakaisha, akaondoka akiniambia kuwa anakwenda kumalizia dawa kwa sababu bado anaumwa miguu, nikamruhusu.

“Cha kushangaza, alipoondoka kuna baadhi ya vitu alichukua kama vile gari, akaniambia analipeleka kwa fundi litarudi lakini mpaka ninavyokwambia huu ni mwaka halijarudi na wala sina mawasiliano naye.”

Ijumaa: “Sasa umepanga vipi na je, bado upo nyumbani kwake?”
Cynthia: “Baada ya kuona nimekaa kwa muda mrefu bila mawasiliano naye niliamua kurudi nyumbani.”

Tujikumbushe kidogo
Cloud na Cynthia walifunga ndoa ya Bomani (kwa mkuu wa wilaya) mwaka 2009, harusi yao ilifanyika kwenye Ukumbi wa Msasani Beach, Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Muvi na wanamuziki mbalimbali

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364