Zijue Hapa Baadhi ya Kazi Alizofanya za Marehemu Kanumba
Aliyekuwa mwigizaji wa filamu za Kibongo,marehemu Steven Kanumba leo ametimiza miaka minne tangu alipofariki dunia April 7 mwaka 2012.
Historia ya Hayati Steven Kanumba.
Amezaliwa: Januari 8 1984 Shinyanga,Tanzania
Amekufa: Aprili 7, 2012 Dar es Salaam,Tanzania
Kazi yakeMuigizaji,Mtunzi,Mtayarishaji,Muongozaji
Steven Charles Kanumba(8 Januari1984,Shinyanga-7 Aprili2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchiniTanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Maisha:
Steven alianza masomo yake katikashuleya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari hukoMwaduina baadae kupata uhamisho katika shule moja jijiniDar es SalaamiitwayoDar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katikashuleya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.
Shughuli za uigizaji:
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya “90”. Ila kufahamika zaidi alianza mwaka2002mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kamaKaole Sanaa Group.
Alijizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na alikuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibunnchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.
Aliweza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeriana pia Wanigeria walipendezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to Lagos,She is My Sisterna nyingine ambazo bado zinajengwa.
Filamu na Tamthilia Alizotunga
1Tufani( Johari )
2Gharika
3Baragumu
4Sikitiko Langu
5Johari 2
6Dangerous Desire
7Dar 2 Lagosi
8Cross my Sin
9Village Pastor
10Family Tears
↑Rudi Sehemu A
Filamu na Tamthilia Alizoigiza
1Jahazi( Tamthilia )
2Dira( Tamthilia )
3Tufani( Johari )
4Gharika( Tamthilia )
5Baragumu( Tamthilia )
6Sikitiko Langu(Filamu)
7Johari 2(Filamu)
8Dangerous Desire(Filamu)
9Dar 2 Lagosi
10Riziki (film)(Filamu)
11Cross my Sin(Filamu)
Chanzo: Cloudsfm.com