CUF Lipumba Yakiri Aliyekatwa Kisigino ni Mlinzi wa Chama
Dar es Salaam. Chama cha Wananchi CUF kimekiri kuwa mtu aliyekatwa kisigino katika vurugu zilitokea Jumamosi iliyopita ni mlinzi wa chama hicho.
Akizungumza leo Mkurugenzi wa Habari wa CUF,Abdul Kambaya amesema mlinzi huyo na wenzake walikwenda Mabibo kwa ajili ya kufanya doria.
Amesema mlinzi huyo Rashid Mtawa alikatwa mapanga na wafuasi wa chama hicho wanaounga mkono upande wa Katibu Mkuu Seif Sharif Hamad.
Amesema si kweli kwamba mlinzi huyo alipigwa na wananchi wenye hasira bali CUF upande wa Maalim Seif.
Amewaomba radhi waandishi wa habari kwa tukio hilo na kusema chama hicho ndicho kimesababisha wapigwe.
“Hata kama sisi hatukuhusika kuwapiga waandishi tunaomba radhi kwa sababu bila kuwepo CUF wasingepigwa.” amesema
Mwananchi