-->

Darasa Atoboa Siri ya Muziki Wake Kukubalika

MSANII wa miondoko ya hip hop nchini, Sharif Ramadhan, amesema siri iliyopelekea nyimbo zake kukubalika ni kutambua wanachotaka mashabiki wa muziki wake.

darasa732

Darasa aliliambia MTANZANIA kwamba katika ushindani wa sasa, msanii hatakiwi kukurupuka, bali anatakiwa atambue mashabiki wake wanataka nini na kwa wakati gani.

“Mwanzo nilikuwa nikitoa nyimbo zenye vionjo vyenye ujumbe wa kutosha lakini hazikuwa zikipokelewa sana ila nilipokaa na kufikiria zaidi, nikatambua nini mashabiki wanataka na ndiyo maana muziki wangu upo juu sana tofauti na zamani,” alisema.

Alisema kitu kingine ambacho kinapelekea muziki kuwa mzuri ni utunzi, mashairi pamoja na kutambua prodyuza anayeendana na unavyotaka muziki wako uwe.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364