Dayna Nyange Afungukia Penzi la Prezzo
Msanii wa Bongo Fleva Dayna Nyange amefunguka kuhusiana na tetesi kuwa waliwahi kutoka kimapenzi na Rapper kutoka nchini Kenya Prezzo na kwamba Prezzo alivunja mahusiano na mpenzi aliye kuwa naye.
Akizungumza na Enewz Dayna amesema kuwa alikutana na Prezo kabla ya yeye kuwa star mkoani Morogoro katika show ambayo yeye alimfata A.Y kwaajili ya project yake ya kimuziki.
“Wakati nipo nao nikatamani kupiga nao picha ya kumbukumbu ambayo baadae mzazi mwenzangu alivyoiona ilikuja kuleta shida hadi ikapelekea tukakosa maelewano na baadaye tukashindwana”, alisema Dayna.
Aidha Dayna akiizungumzia skendo ya yeye kutoka kimapenzi na rapper Roma Mkatoliki ameiambia Enewz kuwa yeye na Roma ni washikaji tuu na ushiriki wake katika harusi ya rapper huyo ni moja ya majukumu ya sehemu ya familia kwani kwa sasa yeye amekuwa ni mmoja wa familia hiyo.
eatv.tv