-->

Daz Baba Amgundua Mchawi Wake

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Daz Baba amedai amegundua kitu ambacho kinamkwamisha ashindwe kufanya vizuri kama zamani.

Daz ambaye amewahi kufanya vizuri na nyimbo nyingi ikiwemo ‘Namba 8’, ameimbia Bongo5 kuwa uwekezaji katika kazi zake za muziki ndio kitu ambacho kinamfelisha.

“Mimi kitu ambacho kinanikwamisha kwa sasa ni video kali. Kwa sababu nyimbo zangu ni kali sana na sijawahi kufanya kazi mbaya katika maisha yangu,” alisema Daz. “Kama ningepata management kali ya kusimamia muziki wangu na kuwekeza ningerudi vizuri kwenye game,”

Aliongeza, “Siwezi kukata tamaa na bado napambana najua bado nafasi ya kufanya vizuri ninayo kwa sababu kila kitu ninacho katika muziki wangu,”

Daz amedai kwa sasa anatafuta management ambayo itasimamia muziki wake.

Rapa huyo ni mmoja kati ya wasanii wa Kundi la Daz Nunda ambao walifanya vizuri katika kipindi cha nyuma.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364