Diamond Akabidhiwa Bendera Kuiwakilisha Tanzania Kwenye AFCON, Gabon
DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo January 14 2016 amemkabidhi nyota wa Afro Pop, Diamond Platnumz bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye ufunguzi rasmi wa mashindano ya Africa Cup of Nation (AFCON) yanayotarajiwa kuanza nchini Garbon hivi karibuni.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, imekuja ikiwa ni baada ya nyota huyo wa muziki kuteuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwenda kutumbuiza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo.