-->

Mama Kanumba: Huyu Ndiye Mrithi wa Kanumba, Naamini Atanifuta Machozi!

DAR ES SALAAM: Wakati ikiwa inakaribia miaka mitano tangu  Aprili 7, 2012, ambapo aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, Steven Kanumba, alipoaga dunia, mama yake mzazi Bi. Flora Mtegoa ametembelea kaburini kwa marehemu mwanaye siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake akiwa ameambatana na kijana aliyemuanika kuwa ndiye mrithi wa muigizaji huyo nambari one nchini.

Katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita, mama huyo alisema siku ya kwanza kuonana na kijana huyo aliyemtaja kwa jina la Fredy Swai, alipatwa na mshtuko mkubwa kwa sababu alimuona anafanana mno na mwanaye, tofauti na watu wengine ambao mara kadhaa wamekuwa wakifananishwa na mkali huyo wa filamu Tanzania.

Fredy ambaye ni msanii wa Tamthilia ya Dhamira inayorushwa katika kituo cha televisheni cha ITV, ameelezewa na mama huyo kuwa anafanana mno na mwanaye na kwamba anaamini atamfuta machozi siku zote za maisha yake.

Akimzungumzia kijana huyo, alisema alipigiwa simu na kuambiwa juu ya mfanano huo na siku alivyokwenda nyumbani kwake Kimara Temboni, aliamini faraja yake iliyopotea imerejea upya.

“Nimeona ninunue kadi niweke kwenye kaburi la mwanangu kumuenzi kwa maombi, sikutaka kusumbua watu ndiyo maana unaona nimeambatana na vijana wangu wawili tu, huyu Fredy tangu nimfahamu najihisi kama namuona mwanangu, nimekubali kuwa wanafanana sana hao wengine sijawapitisha.fredy-mrithi-wa-kanumba-6

“Kila ninapofika hapa kaburini huwa machozi hayakauki, lakini leo ni tofauti na siku zote, chozi langu halijadondoka, sababu nimempata mrithi wake, mtu ambaye ananifanya nisilie tena, nampenda kama Kanumba, naamini atafuata nyayo zake kwenye sanaa,” alisema mama huyo
Wakiwa makaburini hapo, mambo matatu muhimu yalifanyika, ikiwa ni kusafisha kaburi hilo, kufanya maombi ya kumtakia mema huko aliko, sambamba na kuweka shada la maua na kadi kwa kumuenzi.

Kwa upande wake, Fredy alisema, amekuwa akipata usumbufu mkubwa kwa kufananishwa na Kanumba na mara nyingi amekuwa akiitwa jina la Steve, ndipo watu wakamshauri amtafute mama huyo kwa kuamini anaweza kufarijika akimuona.

“Tangu utotoni, watu walikuwa wanawaambia wazazi wangu wanipeleke kwa Kanumba nikacheze kama mdogo wake, nikawa naogopa kuonana naye kutokana na ustaa aliokuwa nao marehemu,” alisema chipukizi huyo.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364