Ukweli wa Nuh na Shilole Mwanza, Huu Hapa
Msanii Nuh Mziwanda ambaye bado anafanya vyema na wimbo wake ‘Jike shupa’ amekanusha tetesi za yeye kuwa pamoja na mpenzi wake wa zamani Shilole jijini Mwanza siku mbili hizi.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, Nuh Mziwanda anasema ni kweli alimuona Shilole Mwanza kwenye club ambayo yeye alikuwa anafanya show na aliambiwa kuwa yupo pale lakini hakukutana naye wala ku-kiss na yeye kama ambavyo watu wanadai kuwa waliwaona wakali hao wakiwa pamoja na waki kiss.
“Mimi nimekuja Mwanza kwenye show zangu nimekutana naye tu Club hivyo mimi siwezi kumkataza mtu kuingia sehemu hivyo hilo ni jambo la kawaida, mimi mwenyewe niliambiwa yupo humu so sikujali maana mimi nilienda kufanya kazi na yeye alikwenda kufanya kazi kimpango wake. Kwa hiyo hayo maneno mengine yanayoongeleka mimi mwenyewe siyajui mimi nimekuja Mwanza kutafuta pesa” alisema Nuh Mziwanda
Mbali na hilo Nuh Mziwanda anasema kwa yeye saizi ni mume wa mtu hivyo hawezi kufanya mambo ya ajabu ajabu kama hayo kwa kuwa yeye anajiheshimu na kuheshimu ndoa yake
“Mimi nimeoa najiheshimu siwezi kufanya vitu ambavyo si vya maadili au ambavyo sitakiwi kuvifanya kilichonileta Mwanza ni kufanya show na kufanya makubaliano na kusaini mkataba wa show yangu nyingine itakayofanyika Dar es Salaam” alisema Nuh Mziwanda
eatv.tv