-->

Diamond Afungukia Mimba Nyingine ya Zari

STAA wa Bongo Fleva asiyechuja kwa takriban miaka 7 mfululizo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameeleza mikakati yake kuwa ana mpango wa kumpa mimba nyingine malkia wake wa nguvu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Risasi Jumamosi linakuhabarisha.

Diamond Akiwa na Zari

Diamond Akiwa na Zari

Diamond ambaye tayari amejaaliwa mtoto mmoja (Tiffah) na mrembo huyo raia wa Uganda, amefunguka jambo hilo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano mafupi na mwanahabari wetu kuhusu mikakati yake ya kimaisha.

Alisema anamshukuru Mungu Zari kukubali kumzalia Tiffah tofauti na warembo wengine aliowahi kutembea nao lakini kwa kuwa yeye anapenda watoto, ameanza ‘kuchakarika’ ili Tiffah apate mdogo wake na si huyo tu, hata na mwingine kadiri Mungu atakavyombariki.

“Mimi napenda watoto. Bahati nzuri Mungu pia amenipa mwenzangu ambaye naye anapenda watoto. Hivyo si vibaya nikifikiria mtoto mwingine na mwingine yani kadiri Mungu atakavyonijalia.

“Yote hayo nitayafanya kwa utaratibu maana si unajua tena shughuli zangu za muziki nazo zinanibana, bado nahitajika nilee familia hivyo nitajipanga vizuri nina imani hakuna kitakachoharibika,” alisema Diamond.

Kabla ya kukutana na Zari, kwa nyakati tofauti Diamond aliwahi kubanjuka penzini na warembo kama Penniel Mungwila ‘Penny’, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Wema Sepetu ‘Madam’ pasipo kupata mtoto ambapo staa huyo wa Wimbo wa Utanipenda akisema warembo hao hawakuwa tayari kumzalia kwa kile alichodai kuwa walizidiwa na nguvu ya ujana.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364