-->

Diamond Afungukia Swala la Zari Kumtembelea Mzazi Mwenzie

Msanii wa muziki, Diamond Platnumz amedai ameshindwa kupost chochote kumtakia hali aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Zari, Ivan ambaye amelazwa hospitali, kwa madai ataonekana anatafuta kiki.

 

Muimbaji huyo amedai amekuwa akimhimiza mpenzi wake Zari kwenda kumtakia hali mzazi mwenzake huyo.

“Ni kweli mzazi wake Zari anaumwa, na yuko serious. Na kila siku huwa namuhimiza Zari akamuone mzazi mwenzie kwasababu najiuliza asingekuwa anaenda familia yangu ingemuonaje, kwa hiyo maskini dada wa watu kila siku huwa anaenda,” Diamonda alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Aliongez, “Sijawahi mpigia simu kwasababu yuko serious sana na pia sikuweza kumpost kwasababu watu waneanza kusema labda natafuta kiki maskini ya Mungu kumbe wala,”

Hivi karibuni Zari alionekana katika picha akimjulia hali ex wake Ivan Ssemwanga ambaye anadaiwa kulazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kupata matatizo ya moyo.

Mitandao ya Uganda inadai kuwa Ivan anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease).

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364