-->

VIDEO: Kala Jeremiah Aumendea Urais

Msanii wa hip hop ambaye anafanya vizuri na hit ya Wananduto Kala Jeremiah amefunguka na kusema hawezi kugombea ubunge kwani tayari ameshafanya kazi hiyo kwa miaka mingi na sasa anasubiri muda ufike aweze kugombea nafasi ya Urais.

Kala Jeremiah

Mbele ya kamera za eNewz Kala amesema kuwa kwa muda mrefu ameshaombwa na wanasiasa mbali mbali pamoja na wananchi ashiriki kugombea nafasi hiyo nzito ya kuwakilisha wananchi lakini bado kwa upande wake haitoshi kwani ameshiriki kuwawakilisha wananchi tangu alipotoa wimbo ‘Wimbo wa Taifa’.

“Nilishaombwa sana kuwa mgombea wa ubunge lakini ukweli tayari nimeshakuwa mbunge kwa miaka mingi lakini kusema tena niende kugombea ubunge haitoshi. Nafasi ya Urais ndiyo nayoitaka lakini siwezi kusema ni lini ila jua ipo siku mimi nitagombea nafasi hiyo”- Kala alifunguka.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364