-->

Diamond Akiri Kupenda Bifu

Msanii Diamond Plutnuz amewashangaza watu baada ya kauli yake kwamba anaona bifu kwenye muziki na kitu kizuri, tofauti na wasanii wenzake wengi ambao hupinga suala la bifu.

diamond332

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond amesema kwake yeye anaona ni sawa tu iwapo wasanii wanakuwa na bifu, kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wao, kwa kuzungumziwa na vyombo vya habari na watu mbali mbali, isipokuwa inakuwa shubiri pale inapogusa familia, na kutoleana maneno machafu.

“Bifu mi naona fresh, kwangu kitu kikizungumziwa ndo naona poa tu kwanza inaniongezea, ila pale inapofikia kugusa kwenye familia na kutoleana maneno machafu ndio inakuwa sio poa”, alisema Diamond Plutnumz.

Kutokana na kauli hiyo, Diamond amekuwa amepigia mstari kuwa wasanii wa lebo yake ya WCB hutegemea ‘kiki’ zaidi kuliko kazi bora kuweza ku-hit, kama ambvyo watu wengi huwatuhumu wasanii hao.

Pia Diamond ametoa siri kuwa mashabiki wake wajiandae mkao wa kula kwani kabla mwaka huu kuisha, atatoa album ambayo itakuwa ya kimataifa.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364