-->

Muigizaji wa Kike Aelezea Maisha Yalivyomfanya Awe Msagaji

Kuna wimbi kubwa la wasichana wanaojihusisha na vitendo vya usagaji.

Malkiz

Malkiz aka Kizz Kiduku ni msanii chipukizi wa filamu Tanzania anayefahamika wazi kujihusisha na vitendo vya kisagaji. Hivi karibuni alikaa na kuzungumza na Global TV na kusimulia jinsi alivyoanza mambo hayo.

Alidai kuwa yote yalianza akiwa shuleni Mwanza ambako kama msichana aliyebalehe alikuwa akipata hamu ya kufanya mapenzi lakini hakuwa na mwanaume wa kuikata. “Nikisikia hamu ya kufanya mapenzi kila nikiangalia nakutana na wanawake,” alisema Malkiz kwa kujiamini na kudai kuwa alilelewa kwenye mazingira ya kukutana na wasichana muda wote ambayo anakiri ilimharibu.

Alienda kusoma Kibaha alikokuwa boarding pia na huko ndio akaanza kujihusisha na vitendo hivyo. “Tukajiingiza kwenye vitu kama hivyo na as days go on nikajikuta nakua na hata nikiwa na wanaume sifeel chochote,” alisema Malkiz mwenye miaka 19 sasa.

Anadai kuwa amewahi kuwa na uhusiano na wanaume zaidi ya 20 lakini bado hakuwa anapata hisia kama mwanamke wa kawaida na kwamba alijaribu kuacha lakini alishindwa.

Anasema hadi sasa ameshakuwa na uhusiano na zaidi ya wanawake 40 na wengine humfuata wao wenyewe.

“Watu wakubwa, miaka 25, 27 kuanzia huko.”

Msichana huyo amedai kuwa wapo wake za watu kibao wanaomtaka na amewahi kutembea na takriban wawili huku akivunja ndoa ya mmoja wao.

 

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364