-->

Diamond ni Mshikaji ila Simtegemei -Shettah

Msanii Shettah ambaye kwa sasa ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Namjua’ amefunguka na kusema kuwa yeye na msanii Diamond Platnumz ni washikaji sana na marafiki wa karibu sana ila inapokuja suala la kazi Shettah anasimama kama Shettah.

Shettah

Shettah alifunguka hayo kupitia show ya Friday Night Live inayorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa na kudai kuwa kwenye masuala ya muziki yeye anasimama kama yeye japo muda mwingine watu hao wamekuwa mchango katika kumbadilisha kutoka kwenye kuchana mpaka sasa anaimba ngoma kama hizo.

“Unajua Diamond Platnumz ni mshikaji sana na mtu wangu wa karibu sana ila inapokuja kwenye masuala ya kazi mimi kama Shettah nasimama mimi kama mimi na ndiyo maana unaona nina Management yangu tofauti na muda si mrefu huenda na mimi nikawa na wasanii nawasimamia kwani kwa sasa siwezi kushindwa kumfanyia msanii kazi na kumtolea pesa ya video lakini nataka nijipange zaidi na team yangu” alisema Shettah

Mbali na hilo Shettah amekiri wazi kuwa katika wimbo wake wa sasa ‘Namjua’ kuna michango ya watu mbalimbali katika kuifanya kazi hiyo isimame na kusema zipo hata melody za Diamond Platnumz ndani ya wimbo huo yaani alimuelekeza labda sehemu hii Shettah pita hivi hapa fanya hivi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364