Diamond Platnumz Afunguka Kuhusu Wema Sepetu
Akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Diamond Platnuzm amesema kitendo alichofanya Wema kupost kazi zake anadhani imefika wakati labda Wema Sepetu ameona hakuna sababu yeye kuendelea kumchukua Diamond Platnumz na ndiyo maana ameonyesha upendo kwa kusupport kazi zake na za wasanii kutoka kwenye Label yake.
“Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekuwa labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa, lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimuwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita” alisema Diamond Platnumz
Mbali na hilo Diamond Platnumz alidai toka ameachana na Wema Sepetu hana namba yake ya simu, hajawahi hata siku moja kumpigia simu wala Wema Sepetu hajawahi kumpigia simu Diamond Platnumz.
eatv