Diana: Nakuja Kwa Kishindo na ‘Kalambati Lobo’
KIMYA kingi kina mshindo ndivyo anavyojinadi mwanadada huyu Diana Kimaro akisema kuwa alikuwa mafichoni akijipanga kwa ajili ya kukabiliana na pacha wake Lulu ili naye aweze angalau kuibuka na uigizaji bora kwa mwaka huu baada ya kufanya kazi zenye ubora mkubwa kwa lengo la kuwa mwigizaji bora wa kike.
“Unajua wengi wanajua kuwa swahiba wangu Lulu anafanya vizuri ndio maana na mimi nilijichimbia sehemu kwa ajili ya kufanya kazi nzuri inipe ushindi sinema ya Kalambati Lobo itatoa majibu kama mimi ni star,”alisema Diana.
Mwigizaji huyo wa kike mwenye makeke katika tasnia ya filamu amesema kuwa mtayarishaji wa filamu ya Kalambati lobo JB alimwamini na kumpa sinema hiyo kwa sababu anajua ataitendea haki sinema hiyo imeongozwa na muongozaji mahiri wa filamu Bongo Rashid Mrutu na kushirikisha wasanii nyota kama Baba James, Tolic na wasanii wengine nyota.
Filamu Central