Nataka Nifanane na Mashabiki Wangu- Man Fongo
Mkali wa singeli nchini Man Fongo amesema hawezi kubadilisha muonekano wake kwa kuwa yeye ni mtoto wa uswazi na anataka kuwa sawa na mashabiki zake.
Akipiga story na eNewz, Man Fongo amesema mashabiki zake ni wale wa uswahilini ambao hawawezi kuvaa nguo ya laki tatu hivyo na yeye hawezi kuvaa hizo nguo bali atavaa sawa na wao ili asiwapoteze.
“Mashabiki zangu wengi wapo uswahilini na sitaki kuvaa nguo za laki tatu zitakazopelekea hata mashabiki zangu washindwe kunisalimia wakiniona na sio kwamba nashindwa kununua hizo nguo za bei ghali” amesema Man Fongo.
Hata hivyo Man Fongo ameendelea kusema kwamba hata gari alilonunua limepelekea baadhi ya mashabiki wake washindwe kumsalimia kwa kwa kumuogopa, Hivyo muonekano wake anautunza kuweka mashabiki wake karibu.
Pia amesema muonekano wake hauzuii kupata wadada warembo kwa kuwa imejengeka kuwa ni lazima kuwa sharo ili uweze kupata wadada tofauti lakini kwa upande wake muonekano wake hauzuii chochote katika maisha yake.
eatv.tv