Machinga Wahahaa Kuitafuta Filamu ya Bei Kali Bongo
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu staa wa filamu Bongo Simon Mwapagata ‘Rado’ amerudi kwa nguvu zote akija na filamu kubwa ijulikanayo kwa jina la Bei Kali, filamu hiyo ambayo imezua simulizi mitaani huku wapenzi wa filamu wakiomba kampuni itakayosambaza sinema hiyo ya Papazi Entertainment iitoe haraka.
Mmoja kati ya wauzaji wa filamu za Kibongo aliyekitambulisha kwa jina moja Athuman kuwa muigizaji Rado sinema zake uvunja rekodi sokoni na kwa muda mrefu hajaingiza filamu zake mtaani hivyo kwa kuja na filamu ya Bei Kali watafanya kazi na kuuza nakala nyingi sana kwani kazi za Kibongo nzuri uuza sana.
“Yaani kila nikienda katika maduka ya kuuza filamu za Kibongo naulizia sinema ya Bei kali ya Rado kila duka haipo jamaa anatunyima pesa hivi hivi, watoe madukani hakuna sinema mpya kila mtu anaisubiria Bei Kali,”alisema Muuzaji huyo.
Filamucentral