-->

Dogo Janja Aponea Chupuchupu Kupotezwa

MSANII wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’ amesema moja ya tukio ambalo hawezi kulisahau kwenye maisha yake ni siku ambayo yeye na washkaji zake walipokwenda kuiba kwenye ‘godauni’ kasha mwenzao mmoja akapotea.

Staa huyo wa singo ya Kidebe, ameliambia Juma3tata kuwa tukio hilo lilitokea zamani wakati anahangaika kutoka kimuziki nyumbani kwao Ngarenaro mkoani, Arusha ambapo yeye na washkaji zake walikuwa wanafanya michongo ya kukaba.

“Kuna siku tulikwenda kuiba sehemu, basi tulipofika kwenye godauni moja hivi ambalo mara kwa mara tulikuwa tunakwenda kufanya yetu ikabidi tumtume mmoja apande juu kwenye ukuta achungulie ili kama kuna chochote tuzame tupige,

“Basi tukamsapoti jamaa wetu mmoja akapanda kwenye ukuta alipoingia ndani tukasikia tu mlio wake mmoja tu kasha kukawa kimya, hapo wote tukakimbia na siku hiyo jamaa hatukumwona sijui nini kilimkuta,” alisema Dogo Janja.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364