-->

Wolper Avunja Kiapo Alichokula

MKALI kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Jacqueline Wolper amevunja kiapo alichokula kwamba kamwe hatamwanika mpenzi wake kwenye mitandao baada ya kujiachia kimahaba bila kuogopa chochote.

Jacqueline Wolper

Siku kadhaa zilizopita, Wolper alipozungumza na gazeti ndugu na hili, Risasi Jumamosi ambapo alisema kuwa, baada ya kuachana na mpenzi wake wa zamani waliyekuwa wakijiachia mitandaoni alisema endapo atapata mpenzi mwingine kamwe hatamwanika, lakini sasa anaonekana kuvunja kiapo hicho.

“Wolper aliapa kwamba hatamwanika tena mpenzi wake, lakini sasa hivi anajiachia kimahaba na huyo Brown na kutupia picha za kimahaba mitandaoni bila kujali alichojiapiza mwanzo,” alisema mmoja wa mashabiki waliosoma gazeti ambalo Wolper alijiapiza. Kwa upande wake Wolper aliruka kujibu ishu hiyo.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364