-->

Sitti Mtemvu: Nilivuliwa Taji La Miss Tanzania Ila Nilikuwa na Umri stahiki (Video)

SHINDANO la Miss Tanzania Mwaka 2014, liliingia kwenye dosari baada ya mshindi wa taji hilo, Sitti Mtemvu kuzua sintofahamu kwa kudaiwa kwamba alishiriki akiwa juu ya umri stahiki wa mashindano hayo. Skendo nyingine iliyomtafuna Sitti ni kudaiwa kuwa alishiriki u-miss huku akiwa na mtoto.

Kutokana na fi gisufi gisu za hapa na pale, hatimaye Sitti aliamua kulivua taji la u-miss na kuvishwa tena mshindi wa pili, Lilian Kamazima. Global TV Online lilifanikiwa kuzungumza na Sitti Mtemvu kuhusu maisha yake baada ya skendo ya Miss Tanzania.

Maisha yakoje baada ya kuvua taji? Mimi niko poa, pamoja na kulivua taji la Miss Tanzania bado niko mrembo kama unavyoniona, maisha lazima yasonge, kilichotokea nilichukulia kama changamoto ambayo nilipaswa kuipitia. Ulifanya nini baada ya kuvua taji?

Niliamua kuandika kitabu changu cha Chozi la Sitti, kitabu ambacho kinaelezea uzoefu na mafunzo yangu niliyoyapata na kuyapitia kwenye sakata la Miss Tanzania.

Kwa nini Chozi la Sitti? Kitabu hiki niliandika kutokana na mapitio yangu kwenye kambi na hata u-miss wenyewe. Ni maumivu makali sana ambayo niliyapitia hata kama angekuwa mtu mwingine angeumia. Lakini baada ya hapo nilianzisha taasisi yangu na kufanya harakati za hapa na pale lakini baadaye nikaenda Marekani kuongeza elimu zaidi. Kwani uliumia kwa kiasi gani? Niliumia sana kwani karibu siku 30,

 

vyombo vya habari vilikuwa ni Sitti, Sitti, iliguswa familia na hata mdogo wangu. Chozi la Sitti nani kakiandika? Kiukweli mwandishi wa kitabu changu ni Mr University wa mwaka 2002, Matukio Chuma.

Yeye ndiye aliyehusika kwa kila kitu kwenye Chozi la Sitti. Ni kweli kwenye Kamati ya Miss Tanzania huwa mnatoa rushwa ya ngono? Si kweli kwamba kamati inaweza kumuingiza mtu kwenye suala hilo la ngono ila ni mtu mwenyewe kwa namna alivyolelewa na kipi alichokifuata

kambini. Wewe ulishawahi kukutana na changamoto ya kusumbuliwa kutoa rushwa ya ngono? Binafsi sikusumbuliwa kwa hiyo siwezi kuwasemea watu wengine.

Nini ushauri wako kwa kamati? Wanapowafanyia mafunzo ya kutembea, kuvaa na namna ya kutembea stejini basi waandaliwe pia kisaikolojia.

Unamaanisha nini? Kipindi cha ushindi wangu kuna warembo hawakuamini na wengine walizimia, wengine wakaniibia viatu na vitu vyangu kwa sababu tu hawakuwa wamejiandaa kushindwa kisaikolojia.

Nini ushauri wako kwa washiriki wa u-miss? Wanapokuwa wanashindwa basi wakubaliane na maisha na wajue kuwa pamoja na kushindwa lakini maisha lazima yasonge.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364