-->

Dokii Afunguka Kumzimia Daraka

Staa wa Bongo Movie, Dokii ameshindwa kuzuia hisia zake za mahaba kwa rapa darassa anayekiki zaidi kwa sasa hapa Bongo na ngoma yake ya Muziki, na kuamua kueleza wazi kuwa anampenda sana.

Dokii ambaye amekuwa kimya muda mrefu kwa kutofanya kazi yoyote mpya ya sanaa, amesema kwa sasa anamkubali sana Darassa kupitia kazi yake ya muziki, lakini yuko tayari kuolewa naye endapo Darassa mwenyewe atahitaji hilo.

Dokii alifunguka ya moyoni akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV kinachoruka LIVE saa 3:00 usiku, na kufafanua kuwa ameamua kuwa mkweli na muwazi kwa kuwa rapa huyo ni mzuri na yeye Dokii kwa sasa hana mtu ambaye yuko naye kwenye mahusiano, lakini mara kadhaa akajikuta akijichanganya kwa kupindisha kauli yake kuwa anampenda Darassa kikazi kama shabiki wake na siyo kimapenzi.

“”Nampenda sana Darassa, i love him, nampenda kwa sababu ya kazi yake, lakini sijawahi kumwambia, he is handsome….Darassa mi nampenda kazi yake but is very handsome, so what do you expect?….. Mie sina mtu kwa sasa, so kama Darassa akitaka kunioa, niko tayari, am ready coz he is handsome”  Sehemu ya alichokisema Dokii kuhusu Darassa

Dokii alikuwa akifafanua kuhusu picha ambayo ameonekana akiwa amepiga na Darassa, picha iliyozua mjadala kutokana na kuwa katika pozi lenye utata.

Pia alifafanua kuhusu mahusiano yake na msanii Rich Mavoko, ambapo alisema Rich ni ndugu yake hivyo hawawezi kuwa wapenzi .

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364