-->

Dokii Atoa Onyo Hili kwa wa Bongo

Msanii Dokii amewataka Watanzania waache kumfuatilia maisha yake, kwani maisha yake hayawahusu hata kidogo, hususani kwa kipindi hiki ambacho ameamua kuokoka.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dokii amesema yeye hajali watu wanachokisema juu yake, kwani anachoangalia yeye ni yale anayoyafanya kwa Mungu wake, hivyo watu wasipoteze muda kabisa kumuongelea.

“Wasiwe busy na mimi na wokovu wangu, acha waongee upuuzi mimi sijali, niko busy na Mungu wangu haijalishi ni msafi au la, sijamwambia mtu nenda club, fanya hivi au ukifanya vile ni dhambi”, alisema Dokii.

Dokii aliendelea kusema kuwa pamoja na yote wanayomuongelea vibaya lakini yeye hayuko hivyo, hata hizo sehemu za starehe anaenda iwapo kuna kazi maalum.

“Sijawahi kwenda club na ndiyo maana watu wanasema hawajawahi kuonana na mimi sehemu za starehe, muda mwengie kama nikienda sehemu ya starehe huenda kuna movie ambayo tunafanya”, alisikika Dokii kwenye Planet Bongo.

Dokii aliendelea kwa kuongelea kitendo cha kuimba wimbo maalum kwa ajili ya ushindi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, na kusema hicho ni kitu cha kawaida kwake kwani hata viongozi wengine alishawahi kuwaimbia.

“Kumuimbia Uhuru Munghai Kenyata si dhambi, siyo yeye tu nimemuimbia Rais Jakaya Kikwete, nimemuimbia Magufuli, nimemuimbia hata Obama alipokuja hapa na watu wakafurahia”, alisema Dokii.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364