-->

Wema Kashaamua, Sasa ni Kazi tu!

SUPASTAA wa Bongo Movie, Wema Sepetu ‘Madame’, ameamua bwana baada ya kuweka bayana kwamba sasa amezama kisawasawa kwenye filamu ili kukata kiu ya mashabiki wake.

Mrembo huyo amesema kuwa kila uchao amekuwa akipokea maoni toka kwa mashabiki, wakihoji ukimya wake kwenye sanaa na amewajibu kuwa watulie wasiwe na kokoro kwani, mambo matamu yanakuja na watakata kiu.

“Kwa sasa sina masihara kabisa katika kazi, nimeamua kufanya mambo na kila kazi nitakayoitengeneza nitaisamba mwenyewe kwa kutumia Mobile App yangu. Sipeleki kwa msambazaji na kusubiria maamuzi yake,” alisema Wema.

Wema alisema anaamini njia hiyo itamsaidia kumnufaisha, tofauti na zamani mfumo ulimkatisha tamaa na kufanya mambo mengine na kuwanyima raha mashabiki wake.

Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 tayari ameandaa kazi mpya iitwayo, Heaven Sent aliyoshirikiana na wakali kama Gabo Zagamba, Neema Ndepanya, Grace Mapunda ‘Mama Kawele’ na mastaa wengine kibao.
Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364