-->

Dude Ajuta Kutofunga Ndoa

MSANII wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa anajuta kutofunga ndoa na mkewe, Eva kwani anateseka sana kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

DUDE34

Kulwa Kikumba ‘Dude’

Akistorisha na gazeti hili, Dude alisema kutokana na sheria za dini ya Kiislamu kwamba hairuhusiwi mwanaume kupikiwa futari na mwanamke anayeishi naye tu bila kufunga ndoa, amekuwa akiteseka kwenye suala la futari kwani mara nyingi anakula kwa mama lishe.

“Najuta kutofunga ndoa na mke wangu maana kila siku huwa nasema nitafunga leo mara kesho lakini miaka imekuwa ikikatika tu sijui kwa nini, kama mwezi huu mtukufu nakula futari kwa mama lishe huku nikiwa nalala chumba cha wageni mpaka mwezi huu uishe,” alisema Dude.

Dude amekuwa akiahidi mara kwa mara kwamba watafunga ndoa na mama watoto wake, Eva  ambaye wanaishi pamoja na wamejaliwa kupata watoto wawili kwamba watafunga ndoa lakini suala hilo limegeuka kuwa kitendawili kwao.

Chanzo:GPL

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364