-->

Dude: Hali Ngumu Imenipoteza Nimeamua Kulima

STAA wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameeleza kuwa kutokana na hali ngumu ya maisha na soko la filamu kuwa gumu amejikuta akiwa kimya na kugeukia kwenye kilimo cha mpunga.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Dude alisema hivi sasa hali imekuwa ngumu sana hasa kwa upande wa sanaa ya filamu jambo ambalo limemsababisha kuwa kimya na kuamua kwenda kulima mpunga huko mkoani Morogoro huku akiendelea kusubiri soko la filamu angalau libadilike.

“Tumelima mpunga na mke wangu Eva maana maisha ni magumu mno, tunamshukuru Mungu ndiyo tunavuna tumepata magunia kadhaa ambayo yatasaidia kuendesha maisha huku nikipambana na tamthiliya mpaka hapo soko la filamu litakapokuwa vizuri,” alisema Dude.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364