-->

He! Nisha kumbe Naye Yumo Buana

STAA wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’ amechomoa kupakaziwa kesi kwa Jacqueline Wolper juu ya kumponda kupenda kwake Serengeti boys (vijana wadogo kimapenzi), akifichua kuwa raha ya wapenzi wa aina hiyo anaijua vema.

Nisha alitupia ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram ambayo ilitafsiriwa na mashabiki wake kama jiwe kwa Wolper, juu ya tabia yake ya kushobokea vijana wadogo na ndipo alipoamua kujitetea kwa kusema hakumlenga yeyote zaidi ya kujisemea mwenyewe.

“Sipendi kinachoendelea sasa, siwezi kumuingilia Wolper katika mahusiano yake, siwezi kumpangia awe na nani ama asiwe na fulani. Raha ya kuwa na Serengeti naijua mimi sema sasa hivi nimestaafu tu na kuiacha, mapenzi yana siri nzito sana,” alisema Nisha.

Nisha alisisitiza kuwa hakumpiga mtu dongo bali ana haki na uhuru wa kuposti chochote katika ukurasa wake kama wafanyavyo wengine, huku akisema kuhusisha maandishi yake na Wolper ni kutaka kumjengea chuki bila sababu.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364