-->

Ester Kiama, Davina Watibuana kisa, Upatu

Mastaa wa filamu Bongo, Ester Kiama na Halima Yahya ‘Davina’ juzikati walitifuana kwa kutupiana maneno makali kupitia kundi lao la Mtandao wa WhatsApp kisa, kikiwa ni mchezo wa upatu.

ESTER23

Sosi ambaye ni memba wa kundi hilo alidai kuwa, wawili hao pamoja na mastaa wengine wana mchezo wao wa kupeana pesa ‘upatu’ lakini siku hiyo Ester akawa amechelewa kutoa, Davina akamtolea uvivu kwa kumchamba.

“Walirushiana maneno makali sana hadi Ester akaamua kujitoa kwenye kundi hilo, yaani ilishangaza sana hadi watu wakahoji ni hizo pesa za upatu au kuna lingine,” kilidai chanzo hicho.

Davina hakupokea simu alipopigiwa lakini Ester alipotafutwa na kuulizwa juu ya habari hizo, alikuja juu akitaka atajiwe aliyevujisha, alipobanwa zaidi akakata simu.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364